Mafunzo ya Utamaduni kwa Wakimbizi

Haki na Mapashwa

Sheria Marekani inafanyika kwa kulinda haki za watu wote ndani mwao wakimbizi. Ni muhimu uwe na ujuzi wa msingi wa haki zako za kisheria na mapashwa yako ufikapo Marekani.

Sheriya ya Amerika: Uongozi wa Sheriya

 • Soma - Sheriya ya Amerika: Uongozi wa Sheriya
  Soma
 • Kusikiya - Sheriya ya Amerika: Uongozi wa Sheriya
  Kusikiya

Sheria za Marekani: Haki za Marekebisho ya Kwanza

 • Soma - Sheria za Marekani: Haki za Marekebisho ya Kwanza
  Soma
 • Kusikiya - Sheria za Marekani: Haki za Marekebisho ya Kwanza
  Kusikiya

Sheria za Marekani 

Kwa sababu Marekani ina tawaliwa na uongozi wa sheriya, kuna sheria nyingi ambazo wakimbizi wanatakiwa kujua. Ni jukumu lako kujua sheria na kuelewa nini ina weza ku tokeya ikiwa unazi vunja.

Marekani, unaweza pewa malipizi ikiwa una vunja sheria, hata kama haukujua kuhusu sheria uliyo vunja. Azabu ya makosa fulani ina weza kuwa kuhamishwa (kurudishwa) kwa nchi yako ya asili. Kwa sababu hio, ni muhimu sana kujifunza naku heshimu sheria.

Kuna aina tatu za sheria Marekani:

Sheria za Jimbo, kama vile sheria kuhusu bihashara na usafirishaji ya vitu, inayo husisha kila mtu anayeishi Marekani.

Sheria za serikali zinatofautiana na jimbo. Kwa mfano, katika jimbo zimoja, unaweza pata  ruhusa yaku endesha ukiwa na miaka 16, lakini kwa jimbo nyingine lazima uwe na miaka 18.

Sheria za mitaa zina husisha kwa kipekee miji ao jimbo. Hizi zinaweza husisha sheria kuhusu ya fujo na shimamisha gari lako.

Ulinzi zidi ya ubaguzi

Sheria ya Marekani inakataza ubaguzi, ijapokuwa maelezo ya sheriya ya kupinga ubaguzi ina pisha na jimbo moja kwa ingine. Ikiwa unabaguliwa  au una imwa haki yako kwa sababu ya rangi yako, dini, jinsia, au asili yako ya kitaifa, una kuwa na haki ya kuchukua hatua yaki sheria.

Hauna hatia hadi itakapooneshwa kosa

Ikiwa una shitakiwa kwa kosa fulani Marekani, una chukuliwa kawa hadi hauna hatia itakapo oneshwa kosa lako. Una kuwa na haki yaku pata muwakili ambaye atakuwakilisha kwenye korti. Ikiwa hauwezi lipa muwakili, korti italipa mumoja aku wakilishe.

Hali yako kisheria na uraia

Hali ya ukimbizi

Kwa mwaka wako wakwanza marekani, utakuwa na hali ya mukimbizi.kwa hiyo muda ina takiwa ku chunga kartasi yako ya I-94 na kitambulisho yako pamoja na picha iliyo kutolewa na serkali kwa wakati wote kama vile ushahidi wa hali yako kisheriya. Ata kama una kuwa na hali ya ukimbizi, hauwezi kusafiri inje ya Marekani bila ruhusa. Weka vikartasi vyako vya awali nafasi nzuri.

Kama mukimbizi, unaweza fanya yafuatayo:

 • Kusafiri popote Marekani. (Kumbuka, uki hama, unatakiwa kujulisha Service ya Immigration ya Marekani (USCIS) kwa siku 10 zinazo fata mabadirisho ya anuwani yako).
 • Kuhuza makao.
 • Kwenda shuleni.
 • Kusaidia mke wako na watoto ambao hawaja funga ndowa wa miyaka chini ya 21. Ikiwa unaitaji mke ao watoto wako  wakukute Marekani, Agence ya Réinstallation lina wezi kukufasiriya yale una takiwa fanya.

Mambo ambalo auwezi fanya wakati unakuwa na hali ya mukimbizi:

 • Hauwezi kupata paspote ya Marekani, kuingiye kwaki jeshi, ku chaguwa kwa uchaguzi, au kutumika katika kazi za serkali ambzo zina omba tu waraiya.
 • Hauwezi safiri inje ya Marekani bila ruhusa kutoka offisi ya wakimbizi na wahamaji wa Marekani (USCIS) shirika ya serkali inayo shimamiya uhamaji.
 • Ikiwa una pashwa safiri inji, Agence ya Réinstallation ina weza ku fasiriya kuhusu namna yaku lomba ruhusa.
 • Ikiwa una rudi kwa inchi yako ya asili ukiwa mukimbizi, unaweza kuto ku ruhusiwa ku rudi tena Marekani.

Ushimikaji wa kudumu

Kisha mwaka mumoja Marekani, unatakiwa kutuma ombi la kugeuka mkaji waku dumu ki sheriya (LPR) au Mteja wa Kadi ya rangi ya majani. Marekebisho haya ya hali ni muhimu sana: inahitajika na sheria na piya ni hatuwa ku pata uraiya wa Marekani.

Kwa maelezo zaidi kuhusu ombi ya uhamaji,  uliza Agence ya Réinstallation na mufanyakazi anaweza kukusaidia au kukutuma kwa mtu anayeweza kukusaidia.

Uraiya

Kisha miaka inne na miezi kenda kama mkaji wa kudumu, unaweza omba uraiya. offisi ya wakimbizi na wahamaji wa Marekani (USCIS) au Agence ya Réinstallation inaweza kukwambia nini una hitaji ile uwe raiya. Zaidi ya yote, unafaa kuonyesha mwenendo mwema na ujuzi wa msingi wa Kiingereza na Historia ya Marekani na serikali. Wahamaji au wakimbizi ambao wamegeuka raiya wanakuwa na haki sawa na faida kama raia waliozaliwa Marekani.

Haki na Mapashwa

 • Lazima usome na ujue sheria.
 • Kila mtu anayeishi Marekani ana haki za msingi kama vile uhuru wa kuongea,uhuru wa kuabudu, na uhuru wa kukusanyika kwa amani.
 • Unaweza fanya kazi Marekani.
 • Raia wanaweza chaguwa katika uchaguzi Marekani.
 • Ubaguzi wa kazi ni kinyume na sheriya Hakuna yeyote anayeweza kataa kukupa kazi kwa sababu ya rangi,dini,jinsia na asili yako ya kitaifa.
 • Kazi za Umma na faida zinapatikana kwa wale wanaostahili kuzipata.
 • Ukivunja sheria hali yako ya uhamaji inaweza husishwa.
 • Unaweza hama kwa shirika
 • Ukihamiya kwa nyumba mpya, ni lazima ujaze kikartasi ya kubadilisha anwani na offisi ya wakimbizi na wahamaji wa Marekani (USCIS).
 • Wanaume wa myaka katikati ya 18 na 25 wana takiwa kuji andikisha kwa uchaguzi wa kazi.
 • Unahitaji kulipa kodi yako muliyo patana. Una takiwa ku jaza na kutuma kartasi ya kodi yako ya mapato kwa serikali kila mwaka. Unaweza kujaza mwenyewe kartasi au kutafuta mtu wakuku saidiya.
 • Unatakiwa kuwa na ruhusa yaku endesha na bima kwaku endesha
 • Watu Marekani wanaweza kosa kunywa au kununua pombe hadi watakapo eneza miaka 21.
 • Wazazi wana takiwa ku soma njia za kisheria zaku azibu watoto wao.
 • Ni kinyume cha sheria kuacha watoto bila mtu mzima wa kuwasimamia.
⇠ Kila kitu kuhusu kufundishwa tabiya za Inchi (Orientation Culturelle)