Mafunzo ya Utamaduni kwa Wakimbizi

Usimamizi wa fedha

Gharama ya maisha Marekani ina pishana sana kwa nafasi moja kwa ingine, ila mahali nyingi ina weza kuwa juu. Ndiyo maana kupata kazi haraka iwezekanavyo ni muhimu sana kwa watu wazima wanaoweza kufanya kazi. Utahitaji kuwa makini sana na pesa zako, ili usitumie zaidi ya unachopata.

Kupangiya Makuta

  • Soma - Kupangiya Makuta
    Soma
  • Kusikiya - Kupangiya Makuta
    Kusikiya

Matumizi ya pesa ki binafsi

Una jukumu la kutumiya pesa yako ya kibinafsi. Njia moja ya kuepuka kutumia pesa nyingi zaidi ni kutengeneza bajeti. Kujifunza jinsi ya kupanga bajeti ni ujuzi muhimu. Kwa kupanga bajeti, ni muhimu kwako kujuwa mapato na matumizi yako ya kila mwezi, kama vile kodi, huduma na mboga. Kwa lengo ya bajeti, itakuwa muhimu kutambua nini jamaa yako inataka zaidi ya kile jamaa yako inahitaji. Vitu fulani vinavyo takiwa vinaweza kuwa vya bei kali na zisizohitajika, na unaweza kuzitoa mbali na mahitaji ya jamaa yako. Wafanyakazi katika Agence ya Réinstallation watakusaidia kupanga bajeti.

Mfumo wa benki 

Mahali salama zaidi pa kuweka pesa Marekani ni benki ambazo zinaongozwa na jimbo na zina kuwa na bima. Kuna aina tofauti za benki. Agence ya Réinstallation itakusaidia kupata benki ambayo inakufaa zaidi. Ikiwa una imani yaki mila au ya kidini kuhusu pesa (kwa mfano ikiwa una amini ni makosa kulipa au kukusanya faida) unaweza kupata benki katika eneo lako ambayo ina fanya imani yako.

Unatakiwa kuelewa namna gani kuweka pesa kwenyi benki na namna ya kuiondoa kwa kutumia Automatic Teller Machine (ATM) au kwa kuandika kartasi ya benki. Kwenye benki, unaweza kuweka pesa yako katika akaunti ya kuangalia na akaunti ya akiba au zote mbili. Akaunti za kuangalia ni nzuri unapohitaji kuweka au kuondoa pesa mara kwa mara ukitumia kartasi ya benki na Automatic Teller Machine (ATM). Akaunti za akiba zina tumika kuchunga pesa ambayo hauhitaji kwa muda. Kwa mara ya kwanza, utahitaji tu akaunti ya kuangalia. Baadaye, wakati unaweza kuchunga pesa, unaweza taka kuwa na zote mbili, akaunti ya kuangalia na ya kuweka akiba.

Unapotumia mpango wa mikopo au kadi ya mkopo, unadai pesa na utalipisha riba kwa kiasi ulichopashwa. Ili kuwa na historia nzuri ya mkopo, lipa mkopo wako kwa wakati kila mwezi. Kufanya malipo ya kila mwezi kwenye mkopo wako wa kusafiri ni nafasi yako ya kwanza ya kujenga historia nzuri ya mkopo.

Kulipa ya moja kwa moja

Washimamizi wengi wana towa au wana hitaji kulipa ya moja kwa moja katika akaunti za benki za wafanyakazi. Katika kuweka  moja kwa moja, malipo yako ina tumwa moja kwa moja katika akaunti yako ya benki kisha kupewa kama hundikartasi ya benki. Kuna faida nyingi ya malipo ya moja kwa moja. kartasi yako ya benki haiwezi potezwa na hakuna yeyote anayeweza kuiba au kujaribu kulipia kwaku pima saini yako. piya, utapokea malipo yako hata kama hauko kazini siku ya malipo na hauhitajiki kusafiri hadi kwenyi benki kwaku tuma kartasi yako ya benki. Kwa mwisho, ukiwa na malipo ya moja kwa moja, pesa yako iko katika akaunti yako na unaweza ipata moja kwa moja. Unapotuma kartasi ya benki wewe mwenyewe, inaweza kuchukua siku moja au mbili kabla pesa itumwe kwenye akaunti yako.

 

⇠ Kila kitu kuhusu kufundishwa tabiya za Inchi (Orientation Culturelle)