Mafunzo ya Utamaduni kwa Wakimbizi

Afya

Hali ya matibabu Marekani si rahisi kuyielewa na inaweza kuwa vigumu ikiwa ni mara ya kwanza. Kumbuka yakwamba wafanyakazi wa réinstallation wanaweza kusaidia kujibu maswali yako na kukupa maelezo zaidi.

Matibabu nchini Marekani

 • Soma - Matibabu nchini Marekani
  Soma
 • Kusikiya - Matibabu nchini Marekani
  Kusikiya
 • Kuona - Matibabu nchini Marekani
  Kuona

Usafi hapa Amerika

 • Soma - Usafi hapa Amerika
  Soma
 • Kusikiya - Usafi hapa Amerika
  Kusikiya

Matibabu Yako Ya Kwanza

Mawasiliano yako ya kwanza na matibabu Marekani inapashwa kuwa iyo siku yako ya kuanza ya uchunguzi wa Matibabu yaki afya. Agence ya Réinstallation yako  ita andaa uchunguzi uho mara unapo wasili. Kupimishwa itaruhusu ku gunduwa shida za ki afya ambazo zina weza kabili réinstallation wako, kama hali yako ya kufanya kazi ama ya watoto wako kuenda shuleni. Watoto wako wanaweza pata immunizations wakati wa kupimishwa kwani, watoto wote wanao ingiya katika shule za ki serkali wana takiwa kuonesha kama wamepata immunizations.

Wanaotowa kazi za matibabu

Kuna aina mbalimbali za wanaotoa kazi za matibabu nchini Marekani. Kati yawanaotowa kazi za matibabu ya kikawaida:

Wizara ya Afya ya Uma utoa immunizations zidi ya magonjwa na tena utoa kazi zingine kwa ajili ya kinga, na izo zavipimo zidi ya magonjua za kifuwa kikuu. Kinga ya huduma ya Afya ni kazi ambazo zina ruhusu kwepuka magonjwa kablaa kutokea. Kwa wakimbizi, kazi izo zina tolewa kwa ujumla bure na azi lipishwi kiyasi. Kukamata mupango kwa jumla ni lazma.

Clinique communautaires na Vituo vya Afya zinatoa kazi za afya za msingi na mashauri ki afya. Wengine utoa matibabu za magonjwa ya meno, na vipimo vya macho. Baadhi ya kliniki katika miji mikuu zina jihushisa kwa kipekehe na hali za wagonjwa kama vile hakina mama wadjawazito ama tena watu wanao hishi na virusi vya ukimwi. Kliniki zinakubali bima ya kibinafsi na aide médicale (Aide Médicale – bima ya serkali kwa watu wasiyo jiweza), na zingine zalipisha kulingana na uwezo ya muteja.

Waganga wa kibinafsi mara wana kuwa waganga wanaotiba magonjwa kwa jumla ama wanganga wajuzi. Waganga wa jumla wanatoa matibabo kwa wote pamoja na ukaguzi wa afya kwa mwaka. Wajuzi utumika katika sekta moja ya matunzo. Wajuzi wamoja utiba kundi la watu kama vile wanawake ama watoto. Wengine ujihusisha na ujuzi katika ma swala ya mwili kama vile roho, macho, ama miguhu. Una kuwa na haja ya kukamata mupango kwa kuhona muganga wa kibinafsi. Mbele ya kuhina muganga wa kibinafsi, una pashwa kwa jumla kuhonesha ya kwamba una weza lipa matibabu ama una bima.

Hospitali zina jadiliyana na wagonjwa wanao kuwa na shida za kipekehe zinazo husu vipimo na msaada wa upasuaji. Kwa kawaida muganga wako atakuongoza kwenye hospitali ambako una weza kubalika kisha kupitishwa kwenye uchunguzi wa dharura. Matibabu kwenye hospitali zina kuwa beyi na kunaweza kuhombwa kuhonesha ikiwa unauwezo wa kulipa ama una bima ili ukubaliki. Kwahiyo, chumba za dharura za hospitali aziwezi kukurudisha kwani auna uwezo ya kulipa.

Vyumba vya Dharura vina jibu kwashida za afya zinazo tokeya ghafla na za hatari. Auna haja yakupata mupango ili ujielekeze kwenye chumba ya dharura. Ila inafasi ambako tayari kuna watu na una weza kungojea muda murefu ikiwa shida yako aina hatari. Matibabu kwenye chumba ya dharura ni ya bei sana. Ikiwa shida yako aiko ya araka unaweza kamata mupangiliyo na kliniki ao na dactari.

Kliniki ya huduma ya dharura zinapatikana katika baadhi ya ya nafasi tunako ishi. Kliniki hizi zina kuweko kwa ajili ya hali za magonjwa  ama vidonda ambavyo vina omba matunzo ya araka ila azina hatari sana ili zipelekwe kwenye chumba ya matunzo ya araka. Ahuna haja ya kuweka mupango.

Hali zako za matibabu ya Afya

Inchini  Marekani, una haki mbili muhimu za  matibabu ya afya. Una haki ya ku pata kutafisiriwa nakulindiwa siri. Elezeya hospital ama mufanyakazi wa kliniki ya kwamba una haja ya mutafsiri wakati una panga kuhonana na munganga wala wakati unapokeya matibabu ya araka. Yote inayo pitikana kati yako na anaye kupa matibabu ni mambo ya siri kulingana na sheriya. Anaye kutoleya matibabu awuzi elezeya ata mwana memba ya jamaa yako, rafiki, ama yule alikupa kazi kuhusu afya yako ikiwa auku mu ruhusu.

Mawazo ya wa Marekani kuhusu afya

Waamerika wengi wana ona dactari mara moja kwa mwaka kwa vipimo vya mwili mzima ili wa juwe kuhusu tatizo zozote za afya kabla haija kuwa mbaya zaidi. wana kwenda kwa mganga wa meno mara pile kwa mwaka ili kuwa na meno safi kwakuji kinga zidi ya tatizo za meno. Waamerika wengi wana amini kuwa magonjwa mengo zina weza ku kingwa kupitiya safi na malisho bora, naku pumuzika vuzuri.

Usafi na usafi waki binafsi

Waamerika wengi uji osha kila siku, wosha meno mara mbili kwa siku, uosha nyele, uweka malashi mara moja, na uwosha mavazi yao mara kwa mara. Duka zauzisha vitu vingi vya usafi vinavyo saidiya watu kwepuka kuhonekana ushafu ama kutoa arufu ya jasho. Usafi wa kibinafsi ina weza ya muhimu kwa ku pata na kulinda kazi yako.

Malisho bora

Kula vema ina mahanisha kula chakula inayo ruhusu kuchunga mwili na hali bora ya afya. Iyo ina mahanisa vile vile kuwa na mipaka kuhusu chakula zinazo sababisha shida za afya na magonjua za hatari ikiwa zi na tumiwa kwa kiwango kikubwa. Chakula izo ni kama zile zinazo kuwa na sukali nyingi, chunvi, na mafuta (kwa mufano: chakula ya ku kalangiwa, bonbons, na vinywaji vya sukali).

Matunzo ya Afya ya Kiakili

Wamerika wanaamini kwamba Afya ya Kiakili ni muhimu kama afya ya kimwili. Afya ya Kiakili ina maanisha namna unavyo waza, unavyo fikiri na kutenda wakati unapo kutana na maisha. Pia inahusu namna unavyoshikilia matatizo. Musaada bora wa afya ni pamoja na matibabu na mtaalamu wa Afya ya Kiakili wakati wa lazima. Ikiwa unaona kwamba maisha ni ngumu sana na huwezi kukabiliana na shughuli za kila siku, unapaswa kushauriana na huduma za Afya ya Kiakili. Agence ya Réinstallation linaweza kukusaidia kupata kazi hizi na kuweka maelezo yako ya siri.

SWALI ZINAZO ULIZWA MARA NYINGI

Je pesa ya matunzo yangu ita lipiwa?

Wakimbizi wote wanao pokelewa marekani  wata pokeya Assurance ya Matibabu inayo lipiwa na serkali kwa muda karibuni wa myezi 8 kisha kufika kwao. Hata kama iyo bima ina funika haja zenu zote muhimu za matunzo, ina weza kuto husisha magonjwa ya meno ao ya macho. Tunaku unga mkono ku pata kazi muda kidogo tu kisha ku fika kwako ili upate Assurance ya Matibabu yaki binafsi kwa bei kupitiya mushimamizi wako wa kazi. Ikiwa una kuwa na ulemavu ao ikiwa unakuwa na myaka zaidi ya 65, serkali ya Marekani itakupa Assurance ya Matibabu bure.

Kazi za haina gani zina patikana kwa wakimbizi walemavu?

Sheriya ya Marekani una chunga na ku saidiya walemavu. Agence ya Réinstallation itaku saidiya ku zunguka naku fikiya kazi zilizo andaliwa kwa wakimbizi walemavu. Assurance ya Matibabu na msaada waki pesa kwa walemavuzina patikana na wakimbizi wana weza kuomba hizo kazi kisha ku fika kwao.

⇠ Kila kitu kuhusu kufundishwa tabiya za Inchi (Orientation Culturelle)