Mafunzo ya Utamaduni kwa Wakimbizi

Kazi

Ajira nchini Marekani

 • Soma - Ajira nchini Marekani
  Soma
 • Kusikiya - Ajira nchini Marekani
  Kusikiya
 • Kuona - Ajira nchini Marekani
  Kuona

Ajira kwa Wanawake Wakimbizi

 • Soma - Ajira kwa Wanawake Wakimbizi
  Soma
 • Kusikiya - Ajira kwa Wanawake Wakimbizi
  Kusikiya
 • Kuona - Ajira kwa Wanawake Wakimbizi
  Kuona

Kazi Marekani ni muhimu sana. Kutafuta, kupata na kulinda kazi ni muhimu kwa ali bora na maisha ya baadaye ya jamaa yako. Ni njia araka ya auto suffisant na ni muhimu kwa kufaulu. Agence ya Réinstallation ita kusaidiya kuingiya kwa mawasiliyano na nafasi za kazi ila wewe mwenyewe utakuwa na jukumu yaku tafuta na kulinda kazi yako. Mara kufika Marekani unatakiwa kuwa tayari kutafuta kazi kwa nguvu.

Kupata kazi 

Watu wazima, wanaume kama wanawake, wa umri ya miaka 18 – 64 na wanao uwezo wa kutumika, wangeli fanya kutafuta kazi umuhimu wao.  Kazi inakuruhusu kujibu kwa haja zako na za jamaa. Musaada wa serkali unamipaka katika kiwango na muda, yahani ni muhimu kupata kazi mara kufika kwako Marekani.

Hiyo aimahanishe kama serkali ao Agence ya Réinstallation ina weza kutolea kazi. Inaweza chukuwa ma wiki ama miezi kwa kupata kazi na una weza hojiyana na fasi nyingi za kuajiriwa. Ungelipashwa kutumika na mutaalamu katika maswala ya kazi kwa kutafuta kazi na kuwasiliyana kwa ajili yaku ajiriwa.

Ungelipashwa kubali kazi ya kwanza ambayo umepata ata kama ahijibu vilivyo hadja zako ama tena ailingani na majifunzo yako ili utengeneze hadisi yako ya kazi na uwanze ku saidiya jamaa yako. Usipo itika kazi unayotolewa, unaweza poteza msaada wa serkali. Mara nyingi watu wengi huomba iyo iyo kazi, yahani ni muhimu kuwa tayari kuitika kazi nyipya kwa kuingiya kwa muelekewo mpya. Kwa kujenga hadisi ya kazi, unatakiwa kubaki kazini kwa muda karibuni wa miezi 6.

Desturi yaku tumika Marekani

Marekani ina julikana kuwa na fasi za bahati kwa wale wanao tumika na bidii. Kwa kupata kazi bora, na inayo lipwa vizuri unatakiwa kujuwa kusema, kwandika na kusoma Kingereza na pengine una takiwa kuwa na ujuzi mpya.  Ikiwa ulitumika kwa sekta fulani kwa inchi yako, ungeli fanya darasa zengine na kupata cherti kabla yaku tumika kwa sekta iyo Marekani.

Wanawake na wanaume wana tumika Marekani. Wanawake ni nusu ya nguvu ya kazi, wana fanya kazi zimoja na wanaume kwa viwango vyote na wanaongoza mara fulani wafanyakazi wanaume.

Marekani, watoto wa miaka 14 na zaidi wanaweza tumika kwa muda lakini saa zakazi na ayina ya kazi wanaweza kufanya ina mipaka. Vijana wengi Marekani wana tumika kwa muda kisha shule, mwisho wa wiki na katika mafungo. Marekani inakuwa na sheria zakukinga wafanyakazi vijan.

Kutumuka Haki na Mapashwa

Marekani, wafanyakazi wana kuwa na haki piya na mapashwa nafasi ya kazi. Unakuwa na haki ya kulipwa kwa ajili ya kazi yako na sheria kuhusu kazi ina kinga wafanyakazi zidi ya hali za hatari za kazi. Ni muhimu piya kulipa kodi yako Marekani.

Musimamizi wako wa kazi awezi kukubaguwa kuhusu hali yako ya mkimbizi ama kukuima kazi, awu cheo kwajili ya miaka yako, ulemavu, hali ya ndoa, kabila ama inchi umetoka, rangi, dini, jinsiya, mambo ya ngono, na mwelekeo wa kijinsiya. Hata hivyo, kazi fulani, kwa upekehe katika serkali, zina pewa tu kwa raia wa Amerika.

Wafanyakazi wana haki ya kutumika katika mazingira inaye epushwa na ubaguzi na unyanyasi. Unyanyasaji wa kingono ni kila hali ya aina yakingono inayo tiya mtu katika hali mbaya nakumu ogopesha na aikubaliki nafasi ya kazi.

SWALI ZINAZO ULIZWA MARA NYINGI

Nitapewa msaada waku pata kazi?

Agence ya Réinstallation itakuweka kwa mawasiliyano na nafasi ya kazi  popote utakaposhimikwa, ila wewe mwenyewe utakuwa na jukumu yaku tafuta na kulinda kazi yako. Kupata kazi Marekani ni muhimu, na pengine kazi yako ya kwanza haitakuwa iyo iyo uliyo fanya kutoka nchi yako ama ya sekta iyo iyo. Ina weza kuwa kazi ambayo ailipi vizuri, ama ya sekta ingine ama tena ina weza kuwa kazi ya muda mfupi ama ya saa zisizo fika siku. Kwa sababu garama ya maisha ni juu Marekani, ni kawaida, na mara nyingi ni muhimu, kwa wanaume na wanawake kufanya kazi inje ya nyumba.

Ninawezaje kupata kazi yangu? 

Uchukuzi wa pamoja inapatikana na fasi nyingi katika miji mikuu Marekani. Katika mwendo wa réinstallation gari azipewi. Hivyo, utatakiwa kutumiya uchukuzi wa pamoja kwa kufika kwa kazi lako la kwanza.

⇠ Kila kitu kuhusu kufundishwa tabiya za Inchi (Orientation Culturelle)